Sunday, August 24, 2014

JACKIE CHAN AWAJIBIKA KAMA MZAZI BAADA YA MWANAE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

MUIGIZAJI maarufu wa filamu za mapigano, Jackie Chan ameeleza jinsi alivyosikitishwa na tukio la mwanae wa kiume kukamatwa na dawa za kulevya.Jackie Chan ametoa tamko lenye maneno mazito ya busara na kueleza kuwa mwanae huyo amemuaibisha sana lakini pia amemuumiza zaidi mama yake mzazi.Akiwa kama mzazi, Jackie Chan ameeleza kuwa yeye pia anapaswa kuwajibika kwa kushindwa kumpa malezi bora mwanae hivyo akachukua nafasi hiyo kwa niaba yake kuomba radhi kwa kilichotokea huku akimtaka mwanae Jaycee kufahamu kuwa amefanya kosa na anapaswa kuwajibika.
Hiki ndicho alichokieleza:
“Niliposikia habari, nilikasirishwa sana. Kama mtu mashuhuri katika jamii, najisikia aibu; kama baba yake, nimesikitishwa sana na ameniangusha. Lakini mtu aliyevunjwa moyo zaidi ni mama yake. Ninatumaini kizazi kinachofuata kitajifunza kutoka kwa kosa la Jaycee. Umefanya kitu ambacho ni kosa na unapaswa kuwajibika na madhara yake. Mimi ni baba yako na siku zote nitakuwa na wewe. Tutaface yaliyombele yetu pamoja.Napaswa pia kuchukua sehemu ya wajibu kama baba, sikukufumfundisha vyema.”
“Kwa hiyo, kwa niaba ya Jaycee na mimi, ninamuomba radhi kila mmoja kwa madhara hasi yote yaliyosababishwa. Asanteni.”
Jaycee, ni muigizaji pia na ameshafanya filamu kadhaa. Baba yake aliwahi kusikika akimwambia kuwa anapaswa kutengeneza pesa yake mwenyewe kupitia filamu zake na sio kumtegemea.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI