Wednesday, October 15, 2014

SEREKALI INACHUKUWA HATUA MBALIMBALI KUDHIBITI MAUJI YA TEMBO

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.
Na Mahmoud Ahmad Arusha.
SERIKALI imesema kuwa inachukua hatua mbalimbali ambazo kudhibiti mauaji ya Tembo wanazidi kuteketea na kuangamia dunia kama ambayo yanafanywa na wachache ambao wanatamaa ya kujipatia utajiri.
Hayo yameelezwa na waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu, kwenye kilele cha matembezi ya kupinga mauaji ya Tembo na Faru yaliyoandaliwa na Chama cha waongoza watalii, TATO, yaliyofanyika jijini Arusha kwenye uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Amesema mwaka 1940 duniani kulikuwa na Tembo milioni 10 , lakini kutokana na kuongezeka kwa mauaji tembo inakadiriwa kuwa mwaka 2014 dunia kutakuwa na tembo 4002 tu na hiyo inashiria kuwa tembo wanauliwa kwa kasi kubwa mno.
Waziri Nyalandu,amesema miaka miwili iliyopita ameshaiagiza Taasisi ya utafiti wa wanyama pori nchini TAWIRI na shirika la wanyama pori la Ujeruman, la Frank fut Zological na wadau wengine wa utalii kufanya sensa ya tembo katika mbuga zote nchini .
Amesema rais Kikwete, alipokuwa mjini London, Uingereza, alikutana na mtoto wa Malkia. Prince Charles, na kueleza kuwa Tanzania imeshapiga marufuku biashara ya meno ya tembo na ghala la meno ya tembo ambalo lina akiba ya tani 130,000,zitalindwa na Tanzania kwa kushirikiana na Uingereza, Umoja wa mataifa ili kudhibiti wizi wa pembe hizo.
Nyalandu, amesema katika kukabiliana na ujangili huo tayari serikali imeshawakamata majangili 15,412, na silaha aina mbalimbali zilizotumika kwenye mauaji ya tembo ambazo ni AK 47 ,na Automatiki rifle ambazo zitateketezwa hivi karibuni kwa kuwa zikiachwa zinaweza kuingia kwenye mikono isiyo salama na kusababisha ujambazi
Waziri Nyalandu, ametumia fursa hiyo kuziomba nchi za China, Japan, Thailand ,Korea ya kusini ,na kaskazini ,Vietnam, kuacha kununua meno ya tembo na pembe za faru ili kuokoa mauaji ya wanyama hao.
Awali mwenyekiti wa Chama cha waongoza Utalii, TATO, Wilium Chamburo, ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwamilikisha wanavijiji waishio kandokando ya hifadhi kumilikishwa maliasili zilizopo ili waweze kusaidia ulinzi na udhibiti wa mauaji ya tembo.

0 comments:

Post a Comment