Thursday, October 9, 2014

SABABU ILIYOPELEKEA MWANASHERIA MKUU KUTIMULIWA KAZI KATIKA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Mhe Said Hassan Said awa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, akichukua nafasi ya Aliyekuwa AG wa Zanzibar Othman Masoud pichani.
*******
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo uliaza rasmi 7, Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI