Jackie Chan
MTOTO wa muigizaji maarufu nchini China Jackie Chan, Jaycee Chan amekutwa na hatia na kufungwa miezi sita gerezani kwa kosa la kutoa hifadhi na kuwaficha watumiaji wa madawa ya kulevya nchini Humo.
Hukumu hiyo iliyotolewa katika mahakama ya jijini Beijing imekuja kufuatia sheria kali juu matumizi yasiyo halali ya madawa ya kulevya.
Jaycee Chan mwenye umri wa miaka 32 aliwekwa kizuizini mwezi August mwaka jana baada ya polisi nchini humo kugundua kiasi cha zaidi ya gramu 100 za bangi zikiwa nyumbani kwake.
Jackie Chan akiwa na mwanae Jaycee Chan.
Jaycee alikiri kosa na kusema ukweli kwa polisi mara tu walipofika nyumbani kwake kwasababu hakujua jinsi ya kukabiliana na masuala ya Bangi na madawa ya kulevya.
Kukiri makosa kwa mtoto huyo wa muigizaji maarufu duniani, inatoa ujumbe muhimu kwa serikali ya China kuwa hakuna mtu mwenye kinga juu ya sheria kali ya madawa ya kulevya nchini humo iliyoanza kutumika rasmi June 2014.
Mbali na kifungo hicho cha miezi 6 Jaycee pia ametozwa faini ya kiasi cha dola 322 kwa kosa hilo.
Baba yake ambaye aliteuliwa na polisi wa China kuwa balozi wa kudhibiti mihadarati mwaka 2009, amesema kuwa kijana wake huyo amempa aibu na kumu huzunisha kwa tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment