Marehemu Kipa Fundi Kipande (wa pili kutoka kushoto waliosimama akiwa na kikosi cha Kivule Veteran kabla ya kupambana na timu ya Pugu Kajiungeni hivi karibuni
TIMU ya Kivule Veteran ya Kitunda, Dar es Salaam inasikitika kutanga kifo cha kipa wake namba moja Fundi Kipande (44) aliyefariki jana nyunmbani kwake Kivule baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kivule Veteran, Peter Mwenda alisema marehemu Kipande atakumbumbukwa mengi aliyofanya na kujitolea kwa hali na mali kuiimarisha timu hiyo.
Mwenyekiti Mwenda alisema marehemu nKipande alitumia muda wake kuwahamasisha wachezaji wenzake kucheza kwa ari na kulinda goli lake anapokuwa uwanjani kila timu yake ilipocheza katika michezo ya kirafiki na mashindano.
Marehemu Kipande aliyesaidiana na Jesse John (mtangazaji wa TBC Taifa)kulinda lango la Kivule Veteran alikuwa kivutio kikubwa manjonjo aliyekuwa anayaonesha alipokuwa golini.
Kutokana na msiba huo shughuli zote za michezo ya kirafiki na mashindano yamesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kila mchezaji na washabiki wa timu hiyo wametakiwa kufika klabu iliyopo karibu na ofisi za mchezaji wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo kusaini kitabu cha maombolezo.
Marehemu Kipande alisafirishwa jana hiyo hiyo kwenda kuzikwa nyumbani kwao Kidodi, Kilombero mkoani Morogoro.
Ameacha mke na watoto wawili wa kike, Mungu ilaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amen.
0 comments:
Post a Comment