Thursday, August 27, 2015

RAIS DK.SHEIN AJUMUIKA NA WANANCHI WA MAKANGALE PEMBA KATIKA SHEREHE ZA MAFANIKIO YA YA MRADI WA HIFADHI YA MISITU YA ASILI (HIMA) ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman alipowasili katika viwanja vya msitu wa Asili wa Ngezi Makangale Pemba kwa ujili ya sherehe za mafanikio ya Mradi wa Hifadhi ya Misitu ya Asili Zanzibar (HIMA).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Ferej alipowasili katika viwanja vya msitu wa Asili wa Ngezi Makangale Pemba kwa ujili ya sherehe za mafanikio ya Mradi wa Hifadhi ya Misitu ya Asili Zanzibar (HIMA)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa wa Misiti ya Asili ya Jamii Rahika Hamad Suleiman akitowa maelezo ya miche ya miti mbalimbali ya matunda ya asili Zanzibar wakati wa maonesho ya Sherehe za Mafanikio ya Mradi wa Hifadhi ya Misitu ya Asili Zanzibar (HIMA) zilizofanyika kisiwani Pemba katika Kijiji cha Makangale Msitu wa Ngezi.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa wa Misiti ya Asili ya Jamii Rahika Hamad Suleiman akitowa maelezo ya matumizi ya majiko ya zamani ya kutumia kunin hadi majiko ya sasa ya kutumia mkaa wakati wa maonesho hayo ya kuhifadhi mazingira ya misitu asili Zanzibar. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa wa Maliasili Asili, akitowa maelezo ya kuhifadhi mazingira kwa kutumia malihafi ya makapi ya mbao kwa ajili ya matumizi ya kupikia wakati wa maonesho hayo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia sabuzi za Asili zinazotengenezwa kwa malighafi ya Pemba ya mti ya Mikaratusi, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mkipi Miliki Co Ltd.ya Mzabarau Takao Pemba. Ndg Mohammed Abdalaah. wakati wa maonesho hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia mikoba ya ukili ya kikundi cha Wanawake cha Gando Hand Craft, na kupata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa kikundi hichi Bi Asia Amour.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia Vitabu vya Utafiti wa Utunzaji wa MMazingira katika meza ya maonesho ya Idara ya Misutu na kupata maelezo kutoka kwa Afisa ya Misitu ya Jamii Bi Miza Suleiman.akitowa maelezo ya tafiti hizo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipanda mti wa Muembe aina ya embe mviringo wakati wa hafla hiyo. 
              Muakilishi wa Ubalozi wa Norway Tanzania TrygveBendiksb, akipanda mti wa mfuu.

Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la CARE Tanzania Paul Daniels, akimkabidhi Ngao ya Heshima Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa utunzaji wa Mazingira ya Misitu ya Asili Zanzibar, wakati wa hafla ya sherehe za mafanikio ya mradi huo zilozofanyika katika kijiji cha ngezi makangale Pemba.  
Mwakilishi wa Ubalozi wa Norway Tanzania Tyrgve Bendiksby akitowa salama za Nchi yake wakati wa hafla hiyo ya Mradi wa HIMA zilizofanyika katika viwanja vya kijiji cha msitu wa ngezi makangale Pemba.
Waziri wa Kilimo na Misitu Zanzibar Mhe Dk. Sira Ubwa Mwaboya akihutubia wakati wa hafa hiyo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kuzungumza na wananchi, akizungumzia mafanikio ya mradi huo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa Meza Kuu wakimsikiliza Waziri wa Kilimo na Masitu akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo.iliofanyika katika viwanja vya msitu wa ngezi kijiji cha makangale Pemba Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Waziri wa Kilimo na Maliasi Zanzibar Mhe Dk. Sira Ubwa Mwaboya ripoti ya Utafiti wa Utunzaji Mazingira ya Misitu ya Asili Mwakilishi wa Ubalozi wa Norway. Trygve Bendiksby kwa Mchango wa Utunzaji wa Mazingira ya Misitu ya Asili, wakati wa hafla ya sherehe za Mafanikio ya Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa (HIMA).zilizofanyika katika Kijiji cha Makangale Ngezi Pemba.
Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar Mhe Sira Ubwa Mwaboya akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ripoti ya Utafiti wa Misitu ya Asili Zanzibar (HIMA) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi ripoti ya Mafaniko ya Utafiti wa Utunzaji wa Mazingira ya Misitu ya Asili Zanzibar mmoja wa Mwananchi wa Shehia 43 zilizofanyiwa Utafiti huo ya Mradi wa (HIMA) Ndg Ali Vuai Haji kutoka Shehia ya Jambiani Unguja. Jumla ya Shia 43 zimefanyiwa utafiti wa mazingira ya Utunzaji wa Misitu ya Asili Zanziar na kukabidhiwa ripoti hiyo na Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Makangale wakati wa hafla ya sherehe za Mafanikio ya Utunzaji wa mazingira ya Misitu ya Asili Zanzibar zilizofanyika katika kijijin hicho na kuzinduliwa ripoti ya utunzaji wa mazingira ya (HIMA).
Wananchi wa Kijiji cha Magangale Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe ya Mafanikio ya Mradi wa Utuzaji wa Mazingira wa (HIMA )hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya msitu wa asili ngezi Pemba.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo na Misitu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar akiwahutubia 
Baadhi ya Viongozi wa Shehia 43 zilizofanyiwa Utafiti wa Mradi wa Hima wa utunzaji wa mazingira ya Asili Unguja na Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar akiwahutubia wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya msitu wa Ngezi Makangale Pemba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali baada ya uzinduzi wa mafanikio ya mradi wa HIMA uliofanyika katika msitu wa ngezi makangale Pemba. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Wawakilishi wa Wananchi wa Shehia 43 za Unguja na Pemba waliokabidhiwa ripoti ya Utafiti ya Mafanikio ya Mradi huo wa (HIMA)
#Zanzi News

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI