Tuesday, December 23, 2014

KANUMBA ANGEKUA MWANASIASA MAARUFU WA CHADEMA!

BABA wa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Charles Kanumba, Charles Kanumba, amesema kuwa anaamini kama mwanaye angekuwa hai hadi sasa basi angekuwa mwanasiasa maarufu nchini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza na Uwazi kwa njia ya simu akiwa kijijini kwao Shinyanga, Charles alisema, japo imepita miaka kadhaa tangu kutokea kwa kifo cha mwanaye huyo, bado anawaza ni namna gani angeweza kuleta maendeleo kwa Watanzania. 
“Mwanangu alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa mwanasiasa tena kwa kupitia tiketi ya CHADEMA. Alikuwa akinieleza mambo mengi ya kisiasa lakini kwa bahati mbaya Mungu alimchukua,” alisema Charles.
Chanzo: GP

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI