Friday, January 9, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGOGO MJINI MHE. ABOOD AMWAGA MISAADA KATA YA BIGWA MOROGORO *PICHAZ*


 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Kuhusu kero Zinazowakabili wakazi wa Kata ya Bigwa Katika Ziara yake ya Kutembelea Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Abood Aliata nafasi ya Kuongea na wakazi wa Mitaa wa Mitaa Mbalimbali inayounda Kata ya Bigwa.Mh Abood alijibu na Kutatua Kero Mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.Mbunge Huyo alitoa Majibu Kuhusu Kero ya Umeme,
Maji ,Barabara na Nyinginezo.Pia Mh Abood alitoa Misaada Mbalimbali iliyogarimu zaidi ya Milioni 20 Katika Kata ya Bigwa.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood akiwa kwenye banda la Mama Lishe maarufu Kama Mama Ntilie Ili Kujionea na kujua  Changamoto Zinazowakabili wamama hao katika kazi yao Hiyo wakati wa Ziara yake ya Kutembelea Kata ya Bigwa Jimbo la Morogoro Mjini
Baadhi ya Misaada aliyotoa Mbunge huyo kwa Wakazi wa Kata ya Bigwa.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikabidhi vifaa Mbalimbali kwa Vikundi vya wakina Mama wanaojihusisha na Shuguli za Mama Lishe Katika Mitaa ya Vituli, Bomela, Korogozo,Mungi, na Mgolole Iliyopo Kata ya Bigwa.
 

Wakazi wa Kata ya Bigwa wakiwa wamemzunguka Mbunge wao

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza Kwa Makini Kero iliyokuwa Ikiwasilishwa na Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mgolole kata ya Bigwa alipotembelea Mtaa huo kusikiliza na Kutatua Kero za Wakazi wa Mtaa Huo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea kwa Msisitizo kuhusu watendaji kushugulikia Kero la wananchi wa Kata ya Bigwa kwa haraka.
Badhi ya Wakina Mama wanaojishugulisha na kazi ya Mama Lishe wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwa Amezungukwa na Vijana wa Kata ya Bigwa wakimweleza Kuhusu kero ya Ajira Na Michezo Ambapo Mbunge Huyo alijibu Hoka Hizo kwa Kuwakabidhi Mpira wa Miguu .Kuhusu Ajira Mh Abood aliwaagiza Vijana Hao Kujiunga kwenye Vikundi vya Kufanya Shuguli za Maendeleo na yeye atawawezesha kwa Kuwapa Mitaji.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa CCM Mtaa wa Misongeni B Kata ya Bigwa Ndugu Omary Iddy aliyemgonjwa alipofika Kumjulia hali.


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa CCM Mtaa wa Misongeni B Iliyopo Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro Ndugu Omary Iddy aliyemgonjwa kwa Muda Mrefu Alipofika Kumpa Pole.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Aliofika Kuhani Msiba wa Bi Nuru Binti Ally Ngozi wa Kata ya Bigwa. 


0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI