Friday, January 9, 2015

FLORA MVUNGI A.K.A 'H-MAMA' AFUNGUKA: 'KUZAA RAHA JAMANI!' *PICHA*

Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’.
********
MSANII wa filamu Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’ amewashinikiza wasanii wenzake wa kike kuzaa mapema huku akiwataka kuingia kwenye hatua ya kuitwa mama na kusema kuzaa kuna raha yake.
Akizungumza na mwandishi wetu, Flora alisema baadhi ya mastaa wamekuwa na dhana potofu kwamba, ukizaa unazeeka na utakuwa hufanyi starehe, jambo ambalo halina ukweli. 
“Mimi nawashauri wazae tu, kuzaa kuna raha yake bwana. Unajua starehe haziishi, kikubwa ni wao kuzaa fasta kisha mambo mengine yanaendelea huku tayari wakiwa wameshaweka ile heshima ya kuitwa mama,” alisema Flora.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI