Saturday, October 11, 2014

HOSPITALI YA AGA KHAN YAADHIMISHA MWEZI WA UFAHAMU WA SARATANI YA MATITI DUNIANI KWA KUTOA BURE HUDUMA YA UPIMAJI

Nembo inayoonyesha utaratibu wa 
uchunguzi wa saratani ya matiti.
Mtaalamu wa Saratani katika hospitali hiyo, Dk.Amyn
Alidina akizungumza na wanahabari kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk.Mustafa Bapumia akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo na maadhimisho hayo.Maofisa wa makambi ya saratani ya matiti wa Saratani 
wakisubiri kuzungumza na akina mama waliofika 
kuchunguzwa matiti yao.
Ofisa wa kambi ya saratani ya matiti, Emmy Shayo (katikati), akichukua maelezo kutoka kwa Furahini Ngwirizi aliyefika katika zoezi la uchunguzi wa matiti. Kushoto ni Ofisa mwenzake, Ilham Mazyun.
Ofisa wa kambi ya saratani ya matiti, Issabela Kahindi (kulia), akichukua maelezo ya mama aliyefika kuchunguza matiti yake. 
Maofisa wa zoezi hilo wakisubiri kuchukua maelezo ya akina mama waliofika kuchunguza matiti yao. Kutoka kulia ni Bertha Mwakapenda, Mwanaisha Dallo  na Stellah Lema. 
Ofisa Mwanaisha Dallo (kulia), akichukua maelezo ya 
dada aliyefika kuchunguza matiti yake.
Wakina mama wakiendelea kuchukuliwa maelezo yao 
na maofisa wa zoezi hilo.
Wakina mama wakisubiri kwenda kumuona daktari 
kwa ajili ya  kuchunguzwa matiti yao.
*********
Dotto Mwaibale

HOSPITALI ya Aga Khan, Dar es Salaam, leo imefanya kambi ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti kwa kuadhimisha mwezi wa ufahamu wa Saratani ya matiti duniani.

Kambi hiyo ya afya imeshuhudia  angalau  watu 200 wakifanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti, pamoja nakupata ushauri nasaha kuhusu saratani ya matiti.

Akizungumza l jijini Dar es Salaam leo wakati wa tukio hilo, Dk. Amyn Alidina, mtaalamu wa saratani katika Hospitali hiyo, alielezea umuhimu wa kupima afya mara kwa mara, jambo ambalo huhakikisha afya njema kwa wote.

“Wengi wetu huchukua mda mrefu bila kutunza afya zetu,aidha kwa kuchelewa sana au kwa kusubiri wakati ambao ili kuwa hai au kurejesha afya yako utahitaji matibabu ya gharama kubwa,”alibainisha na kuongeza kuwa, “Ugunduzi wa ugonjwa wa  saratani mapema unaweza kuwa njia kuu ya kupambana na ueneaji  na madhara ya saratani ya matiti.”

Kambi hiyo ni sehemu ya kampeni ya hospitali hiyo yenye kauli mbiu “Usisubiri hadi Oktoba” iliyolenga kuhamasisha umma kuchukua hatua yakutunza afya zao sasa badala ya kusubiri muda maalumu wa mwaka.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kuna kesi mpya takriban 1,380,000 na vifo 458 000 kutokana nasaratani ya matiti kila mwaka. Wingi wa vifo hivyo (269 000) hutokea katika nchi zenye vipato vya chini na vyakati, ambapo wanawake wengi wenye saratani ya matiti huchunguzwa na kutambuliwa katika hatua za mwisho kutokana hasa na ukosefu wa ufahamu wa kugundua mapema na vikwazo vyilivyopo katika huduma za afya.

Saratani ya matiti kwa kiasi kikubwa sasa ni kansa inayowaadhiri sana wanawake duniani kote , katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea. 

Katika nchi zenye kipato cha chini na kipato cha kati matukio haya yamekuwa yakipanda kwa kasi katika miaka ya mwisho kutokana na kuongezeka kwa umri wa kuishi,kuongeza kwa ukuaji wa miji na kuiga  maisha ya nchi za magharibi.

Dk. Alidina anaelezea kuwa "Bado kuna mtizamo kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kwa ajili tu yamatajiri, lakini tunaona kesi nyingi zaidi katika makundi yote ya kipato.”

"Saratani hii hutokea katika umri mdogo katika nchi zinazoendelea kwa watu wenye takriban miaka 40. Hii ni hali inayoleta wasiwasi. Ninaona karibu kesi  20 katika mwezi na wengi wao ni kati ya  umri wa miaka 29 na42. Uchunguzi na elimu ni njia  muhimu  ya kutambua kesi  mapema.”


Sababu za ugonjwa hatari wa  saratani ya matiti ni historia ya  saratani katika  familia, mfumo wa kazi unaoweza kusababisha kansa ,mfumo wa maisha kama vile uvutaji wa sigara, mfumo wa kula, na historia yamaambukizi ya virusi, na saratani iliopita.

Watu hawa  huhitaji ufuatiliaji wa karibu. Ujumbe muhimu ni kuwa na ufahamu wa mabadiliko katika afya yako na kufanya uchunguzi  mara kwa mara.

"Ni  muhimu sana kwamba elimu iende sambamba na uchunguzi kutokana na watu wengi badowamefungwa na hadithi za kale au  imani, ambayo huwazuia kutafuta matibabu. Kuna mengi zaidi ambayo yanaweza kufanyika ili kufikisha elimu ya afya kwa umma hasa katika maeneo ya vijijini. 

Hii inapaswakuhusisha kampeni za kiserikali zinazolenga kansa kama ilivyofanyika katika siku za nyuma kwa ugonjwa wa Ukimwi na Malaria na zifanyike katika mashule, makanisa, majukwaa ya umma na taasisi za afya. Kampeniisiwalenge tu wafanyakazi wa afya, lakini lazima iwahusishe pia walimu na viongozi wa mitaa katika  jamii  ambao wana  taarifa sahihi kuhusu kansa ya ili wazieneze kwa umma.”

"Ni muhimu kutafuta matibabu ya haraka, ukiona dalili zozote za saratani ya matiti, usisubiri mpaka uwe katika hali mbaya ndio uende hospitali, kwa sababu baada ya kuchunguzwa mapema  unaweza kutibiwa kwa ufanisi," alisema Dk. Alidina.
Chanzo: Habari za jamii

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI