RAPPER kutoka Detroit, Michigan Big Sean amezungumzia album yake ya tatu nakusema wasanii watakao husika ni Nicki Minaj, 2 Chainz na Kanye West. Big anasema ni muhimu Kanye kuwepo kwenye album yake sababu ya mchango aliokuwa nao kwenye muziki na maisha yake.
Kwenye habari nyingine Big Sean ametambulisha application ya simu za Android kwa ajili ya kumtoa mpenzi wako wa awali kwenye picha na kuiweka kwenye Instagram,Facebook au Twitter ikiwa na Ujumbe ‘I Don’t F**k With You’ ambayo ndio nyimbo mpya ya Big Sean katika nyimbo nne mpya alizotoa kutoka kwenye album yake mpya. Baada ya kumtoa mpenzi wako kwenye picha, hakikisha unaweka na hii Hashtag#IDFWU
0 comments:
Post a Comment