MSHAMBULIAJI Luis Suarez alilazimika kutoka kasi uwanjani na kukimbilia msalani wakati mechi ikiendelea, lakini kwa ruhusa ya mwamuzi.
Suarez alifanya hivyo wakati Uruguay ikiwa ugenini inaivaa Saudi Arabia katika mechi ya kirafiki.
Yeye ndiye alikuwa shujaa kupiga krosi safi ambayo ilisababisha bao la kuongoza baada ya beki wa Saudi Arabia kujifunga, lakini wenyeji wakasawazisha baadaye.
Suarez bado anatumikia adhabu ya miezi minne kutocheza baada ya kumuuma Girgio Chiellini wa wakati wa Kombe la Dunia.
Lakini ameruhusiwa kucheza mechi ambazo si za mashindano za kimataifa kama hiyo dhidi ya Saudi Arabia.
0 comments:
Post a Comment