MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth
Michael 'Lulu' ameibuka na kufunguka kuwa
amekerwa na kitendo cha mshiriki wa
Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2013,
Amir Khan Nando kujinadi kuwa aliwahi
kuwa 'mtu' wake kitu ambacho si cha kweli.
Akizungumza juzikati, Lulu alikiri kuwa
Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia
awe 'my baby' wake lakini baada ya
kumshtukia kuwa hana nia nzuri,
alimpotezea kabla hawajazama kwenye
dimbwi la mahaba.
"Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki
kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka
kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz
nilishamgundua nia yake, nimemshangaa
kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa
mpenzi wake labda alivyonitokea na
kumkubalia lakini sikufanya naye chochote
kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme
hivyo," alisema Lulu.
Juzikati, Nando alifanya mahojiano na
Global TV Online ambapo awali alidai
'kutembea' na Lulu lakini alipobanwa zaidi
aliumauma maneno na kudai anampenda
na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa
za kuwa mke (wife material).
0 comments:
Post a Comment