WAFUNGA NDOA WAWE WAMETIMIZA UMRI
UNAOKUBALIKA KISHERIA:
MWANAMKE na mwanaume wawe
wametimiza miaka 18 ili kufunga ndoa.
Hata hivyo mwanamke anaweza kuolewa
akiwa na umri wa chini ya miaka18 lakini
sio chini ya miaka 15 kama atapata idhini
ambayo hutolewa na baba na kama hayupo
ni mama au kama wote wamefariki idhini
itatolewa na mlezi wa binti huyo.
Kama wote wamefariki basi hatahitaji
idhini.
Kuna wakati katika mazingira fulani
mahakama inaweza kutoa idhini kwa binti
kuolewa akiwa na miaka 14 lakini si chini
ya hapa ikiwa ataonekana kwa mfano ana
mimba. Pia mwanaume anaweza
kuruhusiwa na mahakama kuoa akiwa na
umri wa miaka chini ya 18 lakini lakini si
chini ya 16 kama ataonyesha kuelewa
jukumu lake kama mtu mzima.
Lakini hii ni pale ambapo
kuna tatizo kama la kumpa
msichana mimba ndipo mahakama inaweza
ikatoa idhini. Katika ombi la kuoa la SHABIRI
A. M. VIRJI (1971) HCD NO. 407 la Mahakama
Kuu ya Tanzania, mwombaji alikuwa na
miaka 16 lakini alimpa mimba binti wa
miaka 18.
Mahakama katika kuchunguza
ombi la mvulana la kuoa ilitoa kibali kwa
sababu wote wawili walipendana sana na
wazazi wao hawakuwa na kipingamizi cha
wao kuoana.
MFUNGISHAJI NDOA KUTOKUWA NA
MAMLAKA:
Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi
kuwa anayewafungisha ndoa hana
mamlaka hayo na kwa makusudu
wakakubali awafungishe ndoa basi ndoa
hiyo itakuwa ni batili.
Mfungishaji ndoa ili
kuwa na mamlaka anapaswa kusajiliwa na
Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa leseni ya
kufungisha ndoa.
0 comments:
Post a Comment