MWANAMKE mmoja nchini Indonesia
amejifungua mjusi badala ya mtoto.
Mwanamke huyo Debi Nubatonis, mwenye
umri wa miaka 31, ameanza kupata vitisho
kutoka kwa kundi la vijana kutokana na
kitendo hicho wakimtuhumu kwa uchawi
ambapo sasa mamlaka za nchi hiyo
zimetuma timu ya wataalamu kwa ajili ya
kumaliza utata wa tukio hilo lisilo la
kawaida.
Wanasayansi katika timu inayofanya
uchunguzi kwa mwanamke huyo
wamesema wanahitaji kupatiwa muda wa
kutosha kuchunguza tukio hilo na kuja na
maelezo ya kueleweka.
Kitendo hicho cha mwanamke kujifungua
mjusi badala ya mtoto kilibainishwa na
mkunga anayedai kwenda nyumbani kwa
mwanamama huyo kumsaidia kujifungua
katika kijiji cha Oenunto kwakuwa
alishindwa kufika hospitalini.
Madai ya mwanamke huyo kujifungua mjusi
yameibua vitisho dhidi ya mwanamke huyo
na familia yake ambao wanatuhumiwa kwa
uchawi na kuamsha mjadala mkubwa
katika mitandao
0 comments:
Post a Comment