Saturday, June 7, 2014

DAVIDO NDIYE MFALME WA TUZO ZA MTV MAMA, MAFIKIZOLO KUNDI BORA, DIAMOND KAPUNI: SOMA LIST NZIMA HAPA!

Davido aliyechukua tuzo 2 mwaka huu!
KATIKA tuzo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, matarajio ya wengi ni kuwa mwakilishi toka Tanzania Naseeb Abdul maarufu kama Diamond angeibuka kinara kwa kuwa ndiye mshiriki aliyekuwa katika vinyang'anyiro kadhaa.
Lakini waswahili husema Mbuzi wa maskini hazai, je ndicho kilichomtokea Diamond, La hasha ni mashindano tu na siku zote lazima mshindi apatikane. Hivyo hakuna ndumba wala dawa katika hilo.
Mashindano hayo yanayoletwa na jimbo la KwaZulu-Natal na kupewa sapoti na Absolut na jiji la Durban, ambapo yalifanyikia katika ukumbi wa kimataifa wa Durban na wasanii kibao toka Afrika na Marekani kwa ujumla walitumbuiza; Fally Ipupa, Michael Lowman, Don Jazzy, DJ Clock, Beatenberg, DJ Kent, Big Nuz, Toofan, D’Banj, DJ Vigi, DJ Tira, DJ Buckz, Burna Boy, Sauti Sol, Ice Prince, Sarkodie, The Arrows, Khuli Chana, Dr Sid, French Montana, Miguel, Trey Songz, Davido, Uhuru, Mafikizolo, Oskido, Professor, Tiwa Savage, Flavour, Diamond, Phyno na Yuri da Cunha.
Davido, Mafikozolo, Uhuru na Clarence Peters ndio walikuwa ni washindi wakubwa usku wa kuamkia leo ambapo Maikizolo walipata tuzo ya kundi bora la mwaka wakati Davido alichukua zawadi mbili moja ikiwa ni Msanii bora wa kiume wa mwaka na msanii bora wa mwaka
Diamond ambaye amekosa tuzo usiku wa kuamkia leo, Usikate tamaa brother, 1 day yes
WASHINDI WA 2014 MTV AFRICA MUSIC AWARDS
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Female: Tiwa Savage (Nigeria)
Best Group: Mafikizolo (South Africa)
Best New Act: Stanley Enow (Cameroon)
Best Live Act: Flavour (Nigeria)
Best Collaboration: “Y-tjukutja” – Uhuru Ft. Oskido, DJ Bucks, Professor and Yuri Da Cunha (South Africa/Angola)
Best Hip Hop: Sarkodie (Ghana)
Best Alternative: Gangs of Ballet (South Africa)
Best Francophone: Toofan (Togo)
Best Lusophone: Anselmo Ralph (Angola)
Artist of the Year: Davido (Nigeria)
Song of the Year: “Khona” – Mafikizolo ft Uhuru (South Africa)
Best Video: Clarence Peters (Nigeria)
Best Pop: Goldfish (South Africa)
Best International: Pharrell
Personality of the Year: Lupita Nyong’o (Kenya)
MTV Base Leadership Award: Ashish J. Thakkar (Tanzania)

Transform Today Award by Absolut: Clarence Peters (Nigeria)

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI