Saturday, June 7, 2014

RIHANNA AHUDHURIA TUZO ZA FASHION ZA CFDA AKIWA NUSU UCHI

Rihanna amewaacha midomo wazi watu wengi baada ya kuonekana amejitoa ufahamu na kuhudhuria tuzo za mitindo (CFDA 2014) zilizofanyika New York akiwa amevalia vazi linalomuacha  nusu mtupu.
Vazi hilo lilionesha wazi kifua chote cha mwimbaji huyo huku maziwa yote yakionekana bila wasiwasi huku akifunika sehemu za chini na kimdoli alichokuwa ameshikilia.
Baada ya kuonekana hivyo katika red carpet, Rude Girl RiRi alipanda na kivazi hicho jukwaani wakati anakabidhiwa tuzo na mhariri mkuu wa jarida la vogue, Anna Wintour.

“Growing up fashion was a defense mechanism. As a child I remember saying: she can beat me but she can’t beat my outfit.” Alisema Rihanna wakati anapokea tuzo yake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI