Saturday, May 17, 2014

MAMA SALMA KIKWETE ALIPOTEMBELEA SHULE YA SEKONDARI SALMA KIKWETE HUKO KIJITONYAMA

Afisaelimu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Omath Sanga akisoma taarifa ya elimu ya wilaya kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati Mama Salma alipoitembelea Shule ya Sekondari Salma Kikwete iliyoko Kijitonyama tarehe 17.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Salma Kikwete wakati alipoitembelea shule hiyo tarehe 17.5.2014.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyoko Kijitonyama wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ndiye mlezi wa shule hiyo wakati alipoitembelea tarehe 17.5.2014. 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma ya asili iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Salma Kikwete iliyoko Kijitonyama katika Wilaya ya Kinondoni. Mama Salma aliitembelea shule hiyo tarehe 17.5.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kinondoni, walimu, wafanyakazi na uongozi wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Salma Kikwete mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali katika shule hiyo terehe 17.5.2014.
Picha na John Lukuwi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI