Tuesday, April 1, 2014

MALI ASILI NA UTALII YAFANIKISHA KUPUNGUZA UJANGILI KWA ASILIMIIA 58, WAKAMATA MENO YA TEMBO,NA MIZOGA YA TEMBO 39

NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA
WIZARA ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana na wadau wengine hapa nchini wamefanikiwa kuendesha doria ambayo iliweza kufanikisha kupungua kwa kasi ya ujangili hapa nchini kwa asilimia 58 tofauti na mwaka jana ambapo ujangili ulikuwepo kwa kiwango cha juu sana.

Aidha doria hiyo ya Mandays pia iliweza kufanikisha kukamatwa kwa mali gahafi ambazo zilikuwa zkitumika na majangili hayo ambayo yamekuwa yakisababisha madhara makubwa sana kwa taifa la tanzania Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Mkurugenzi wa idara ya wanyama pori taifa Paulo Sarakikya alidai kuwa oparesheni hiyo ilianza rasmi toka januarya hadi kufikia mwezi machi mwaka huu na takwimu zinaonesha mafanikio makubwa sana kwani doria hiyo pia iliweza kuhusisha ujangili wa ndani na hata ule wa nje ya hifadhi.

Aliendelea kwa kusema kuwa katika kipindi husika jumla ya mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani na nje ya hifadhi za taifa na mapori ya akibanchini huku meno mazima yakiwa ni 171 na vipande 22 vya meno ya tembo ghafi , vipande 302 vya meno ya tembo yaliyochakatwa yenye jumla ya kilo 662.62 pamoja na nyama pori zenye jumla ya kilo 1,111 ambazo nazo zilikuwa ni kwa ajili ya vitoweo vya majagili hayo.

Sarakikya alidai kuwa mbali na kukamata vitu hivyo pia waliweza kukamata vitu vingine kama vile:
bunduki ya rashasha moja, Rifle 3, shotgun 2, gobori 5 na jumla ya risasi 7 za aina mbalimbali pamoja na malighafi kama vile magari 5 ngombe 2663 misumeno 1 na mbao 745
kutokana na hilo pia watuhumiwa waliweza kulipa faini ya zaidi ya milioni 25 na pia hali hiyo iliweza kusababisha hata ujangili kushuka kwa kiwango cha asilimia 58 tofauti na mwaka jana ambapo ujangili ulikuwa ni mkubwa sana.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI