Tuesday, March 25, 2014

HATIMAYE RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AWASILI ARUSHA KWA KUTUMIA USAFIRI WA BARABARA YA KENYA - TANZANIA.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta jana alisafiri kuelekea mkoani Arusha nchini Tanzania kwa usafiri gari kwa njia ya barabara, safari ya umbali wa kilometa 230. 
Rais Kenyatta alisimama katika maeneo kadhaa kabla ya kuvuka mpaka wa Namanga kwa kutumia kitambulisho kipya kinachoruhusu wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia kusafiri baina ya nchi hizo kwa urahisi. 

Akiwa Arusha, Rais Uhuru atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako atapokelewa na katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Richard Sezibera. 
Siku ya Jumanne anatarajiwa kulihutubia bunge la Jumuiya hiyo kwa wadhifa wake wa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa sasa. Anatarajiwa kusisitiza mshikamano na ushirikiano baina ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. 








0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI