Tuesday, March 25, 2014

MAJINA WA VIONGOZI WA KAMATI 12 ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA NA KAMATI YA UONGOZI YATAJWA


Na Magreth Kinabo, Maelezo - Dodoma 
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samwel Sitta leo, ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.

Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika (jana) Machi 24 , mwaka 2014 mjini Dodoma .

Mwenyekiti huyo aliyataja majina hayo katika Kamati ya Uandishi Mwenyekiti Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni Prof. Makame Mbalawa.

Wengine waliochaguliwa katika Kamati Na. 2 Mwenyekiti ni Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wake ni Shamsa Mwangunga.Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma MussaJuma.

Mhe. Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni Christopher Ole-Sendeka, Makamu wake ni Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni Assumpter Mshama.

Viongozi waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti Stephen Wassira na Makamu wake ni Dkt. Maua Daftari. Kamati Na. 7 Mwenyekiti Brig. Hassan Ngwilizi, Makamu wake Waride Bakari Jabu. Kamati Na. 8 Mwenyekiti ni Job Ndugai, Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.

Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh, Makamu wake Wiliam Ngeleja, Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin.Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni Anne Malecela, Makamu wake Hamad Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti Paul Kimiti na Makamu wake ni Thuwaybah E. Kisasi.

Wakati huohuo, Sitta alitangaza wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba, ambao ni wenyekiti na makamu wenyeviti wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua.

Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na Hamad Abuu Juma.
Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na katika nafasi hiyo .

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI