Polisi wamesema walikuwa njiani kwenda kutawanya watu ufyatuaji wa risasi ulipotokea.
Watu 16 wamejeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi katika bustani moja mjini New Orleans, polisi wamesema.
Msemaji wa polisi Tyler Gamble amesema maafisa wa polisi walikuwa njiani kuvunja mkusanyiko mkubwa wa watu katika bustani ya Bunny Friend Park mjini pale risasi zilipofyatuliwa.
Ambiulensi ziliwapeleka watu 10 hospitalini, Bw Gamble alisema, na wengine walikimbizwa hospitalini kwa kutumia magari ya kibinafsi.
Bado haijabainika ni nini kilichoanzisha ufyatuaji huo wa risasi au kiwango cha majeraha waliyopata majeruhi.
Kwa mujibu wa Bw Gamble, kulikuwa na makundi mawili kwenye bustani hiyo. Kundi moja lilikuwa limeenda kwenye bustani hiyo likiwa kwenye gwaride la wakazi wa mtaa na jindine lilikuwa likishiriki au kutazama video iliyokuwa ikiandaliwa kwenye bustani hiyo.
Walioshuhudia waliambia kituo cha televisheni cha WWL kwamba kulikuwa na watu takriban 500 kwenye bustani hiyo na kwamba watu wawili walianza kufyatulia watu risasi.
#BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment