Mwanadada
aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki,
Rehema Chalamila ‘Ray C’ akihojiwa na wandishi wa habari wakati wa
kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na
usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
Na Andrew Chale, Modewjiblog, Bagamoyo.
***********
MWANADADA
aliyewahi kung’ara katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, Rehema
Chalamila ‘Ray C’ amesema moja ya sababu iliyomfanya kuanzisha taasisi
yake ya kupambana madawa ya kulevya ya Ray C Foundation, ni kutaka
kuelimisha vijana na jamii nzima juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za
kulevya na athari zake.
Ray
C alieleza hayo wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi
ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu maadhimisho yaliyofanyika
Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 26 huku Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
mgeni rasmi kwenye kilele hicho.
Ray C alibainisha kuwa kwa sasa kupitia taasisi hiyo tayari ameweza kusaidia vijana mbalimbali kuachana na dawa za kulevya.
Pia
kupitia taasisi yake hiyo, vijana mbalimbali wameanza kubadili tabia
ikiwemo kuanza kutumia dawa za kuachana na matumizi ya dawa za kulevya
aina ya Methadoni.
“vijana
zaidi ya 70, wameweza kubadili tabia ikiwemo kuanzishiwa matumizi ya
dawa maalum za kuachana na uteja yaani dawa za Methadone.” Alibainisha
Ray C.
Aidha,
kwenye maadhimisho hayo Ray C aliomba wazazi kusaidia vijana wao waweze
kuwapeleka kupatiwa matibabu ya kuachana na dawa za kulevya katika
vituo vilivyopo hapa nchini ikiwemo Mwananyamala, Temeke na ama
kuwasiliana na vituo vya Soba vilivyopo kote nchini.
Mwanadada
aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki,
Rehema Chalamila ‘Ray C’ akihojiwa na wandishi wa habari wakati wa
kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na
usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
Mwanadada
aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki,
Rehema Chalamila ‘Ray C’ akiwa na mmoja wa maafisa wa taasisi yake
wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za
kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
0 comments:
Post a Comment