Sunday, June 28, 2015

RAY C FOUNDATION YASAIDIA VIJANA ZAIDI YA 70 KUACHANA MADAWA YA KULEVYA

DSC_0087
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akihojiwa na wandishi wa habari wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
Na Andrew Chale, Modewjiblog, Bagamoyo.
***********
MWANADADA aliyewahi kung’ara katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema moja ya sababu iliyomfanya kuanzisha taasisi yake ya  kupambana madawa ya kulevya ya Ray C Foundation, ni kutaka kuelimisha vijana na jamii nzima juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya na athari zake.
Ray C alieleza hayo wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu maadhimisho yaliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani Juni 26 huku Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mgeni rasmi kwenye kilele hicho.
Ray C  alibainisha kuwa kwa sasa kupitia taasisi hiyo tayari ameweza kusaidia vijana mbalimbali kuachana na dawa za kulevya.
Pia kupitia taasisi yake hiyo, vijana mbalimbali wameanza kubadili tabia ikiwemo kuanza kutumia dawa za kuachana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya Methadoni.
“vijana zaidi ya 70, wameweza kubadili tabia ikiwemo kuanzishiwa matumizi ya dawa maalum za kuachana na uteja yaani dawa za Methadone.” Alibainisha Ray C.
Aidha, kwenye maadhimisho hayo Ray C aliomba wazazi kusaidia vijana wao waweze kuwapeleka kupatiwa matibabu ya kuachana na dawa za  kulevya katika vituo vilivyopo hapa nchini  ikiwemo Mwananyamala, Temeke na ama kuwasiliana na vituo vya Soba vilivyopo kote nchini.
DSC_0082
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akihojiwa na wandishi wa habari wakati wa kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.
DSC_0066
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’  akiwa na mmoja wa maafisa wa taasisi yake wakati wa  kilele cha siku ya Kimataifa kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji, iliyofanyika Juni 26, Bagamoyo-Pwani.

No comments:

Post a Comment