Mr Blue byser ameamua kuweka wazi ni jinsi gani mke wake amemsaidi
katika kuacha kutumia vilevi vya aina yoyote, na ashukuriwe mke wake kwa
kuwezesha hilo.
Blue kupitia Instagram yake, hit maker huyo wa ‘Pesa’ amekiri kuwa sasa
ana furaha zaidi baada ya kufanikiwa kuacha kuvuta bangi, sigara (fegi)
mirungi na pombe. Amemshukuru mama mtoto wake aitwaye Wahyda kwa
kumuwezesha kuacha kutumia vilevi hivyo.
Hiki ndicho alichokiandika Blue:
“Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu
..na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani ahsante mke
wangu@wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi,
fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri
ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya
kukuharibia maisha yako ..kuwa makini
0 comments:
Post a Comment