Sunday, June 14, 2015

MAPENZI YANA NGUVU: MR BLUE AMSHUKURU MKEWE ‘WAHYDA’ KWA KUMSAIDIA KUACHA KUTUMIA BANGI, SIGARA, MIRUNGI NA POMBE *PICHA*

Mr Blue byser ameamua kuweka wazi ni jinsi gani mke wake amemsaidi katika kuacha kutumia vilevi vya aina yoyote, na ashukuriwe mke wake kwa kuwezesha hilo.
Blue kupitia Instagram yake, hit maker huyo wa ‘Pesa’ amekiri kuwa sasa ana furaha zaidi baada ya kufanikiwa kuacha kuvuta bangi, sigara (fegi) mirungi na pombe. Amemshukuru mama mtoto wake aitwaye Wahyda kwa kumuwezesha kuacha kutumia vilevi hivyo.

http://i1.wp.com/www.bongo61.com/wp-content/uploads/2015/06/Mr-blue.jpg

Hiki ndicho alichokiandika Blue:
“Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu ..na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani ahsante mke wangu@wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi, fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia maisha yako ..kuwa  makini

No comments:

Post a Comment