Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali(PAC) amewasilisha ripoti ya sakata ya Escrow katika mkutano wa 16/17,kikao cha 17 bungeni Dodoma.
ZITTO:
Kamati imebaini kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua yenye Kumb Na. AGCC/E.080/6/70 ya tarehe 18 Novemba, 2013 alimthibitishia Gavana kuwa hakukuwa na kodi ya Serikali katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW na kwamba fedha hizo zihamishiwe IPTL ili Serikali ijinasue na mashauri yasiyo na tija kwake.
Kutokana na mahojiano kati ya Kamati na Kamishina Mkuu wa TRA ilibainika kwamba Kampuni ya Piper Links haijulikani sio tu British Virgin Islands bali hata nchi nyingine.
Kamati haielewi ni jinsi gani taasisi kubwa kama Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nyingine zilizohusika katika suala hili, na ambazo tunaamini zimesheheni Watendaji wenye weledi, zimewezaje.
Wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Novemba, 2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na makubaliano wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au fedha yote katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma.
FILIKUNJOMBE:
Kamati imethibitisha bila chembe ya mashaka kwamba mchakato mzima wa kutoa fedha katika akaunti ya Tegeta ESCROW uligubikwa na mchezo mchafu na haramu wenye harufu ya kifisadi ulioambatana na udanganyifu wa hali ya juu ambao kwa kufuata sheria tu ungeweza kugundulika na kuzuiwa.
0 comments:
Post a Comment