Thursday, November 27, 2014

BUNGE LA ULAYA KUJIENGUA GOOGLE

BUNGE la ulaya linajiandaa na upigaji kura juu ya kujiengua katika upakuaji wa habari zake za ndani katika  huduma za biashara za google.
Bunge hilo limesema kuwa kujiengua na huduma hio ndio njia pekee ya mwisho ya kutatua mgogoro ulikuwepo kwa mda mrefu ambao uliweza kuchunguzwa kwa miaka minne  na kushindwa kufikia muafaka.
Wanasiasa wakubwa Marekani wameonesha kutokubaliana na pendekezo hilo na kuandika barua kwa umoja wa ulaya juu ya kulenga teknolojia ya Marekani wakidai kutapunguza masoko ya google ya nje.
Mapendekezo hayo  yameonekana kujenga ukuta badala ya daraja katika kuleta mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya Marekani na umoja wa ulaya.
Hata hivyo Shirika la mawasiliano limeeleza kuwa kuongezeka huko kwa mambo ya kisiasa katika ushindani wa kibiashara kupitia huduma za google umeonekana kuwa katika matatizo hivi sasa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI