Thursday, November 27, 2014

WAPENDA SELFIE KOREA KUFUNGWA MIAKA 3 JELA...SOMA CHANZO HAPA! *PICHAZ*

WATU walioathirika na upigaji picha kwa kutumia fimbo yenye camera ya mbele maarufu kama Selfie Korea ya kusini,  wanaweza kujikuta wanalipa fine ya dola 27000 au miaka mitatu jela kutokana na wauzaji na wasambazaji wa kifaa hicho cha fimbo ya kupigia picha kutosajiliwa na wizara ya Sayansi ya nchini humo.
Kutokana na Wizara ya sayansi kutoa tangazo hilo huko Korea ya Kusini,  inaonekana adhabu hiyo itamuhusu yule anayeuza kifaa hicho ambacho hakijasajiliwa huku mtumiaji akikumbana na fine ya dola 27,000 au miaka mitatu jela.
Harakati za kusimamisha uuzwaji wa kifaa hiki kidogo ambacho kimetengenezwa kwaajili ya simu ili kurahisisha upigaji picha hazitokuwa rahisi kutokana na Korea ya Kusini kuridhia technologia hiyo kwa shauku kubwa.
Wizara inasema tatizo  ni kwamba muundo wa kifaa hicho kimeundwa kwa kifaa cha mawasiliano ambacho hutumiwa na mawimbi ya radio katika kusambaza taarifa mbalimbali.
Wizara imewataka wasambazaji kupima na kuthibitisha kuwa vifaa hivyo  havitoathiri vifaa vinavyosambaza mawimbi ya radio

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI