LICHA ya jitihada zinazofanyika kutoa elimu ya uzazi salama kwa
wanafunzi bado idadi ya wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni
imeendelea kuongezeka takwimu za mwaka 2010 zikionyesha kuwa watoto wa
kike elfu nane wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini
walikatiza masomo baada ya kupata ujauzito usiotarajiwa.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya uzazi salama duniani
ambayo shirika la Marie Stopes nchini iliadhimisha kwa kutoa elimu kwa
makundi mbalimbali ya vijana, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa shirika
hilo Bwana Johnbosco Basso anasema kuongezeka kwa idadi hiyo pia
kunachangia kuongezeka kwa vifo kutokana na walio wengi kujaribu
kuharibu mimba.
Hata hivyo baadhi ya kinamama wakazi wa Arusha wakizungumzia
changamoto hiyo wanasema pamoja na kuendelea kutoa elimu mashuleni ipo
haja pia wazazi kuchukua jukumu la malezi na ikiwezekana kurejesha
utamaduni ulikua ukitumika awali wa kuwa na kipindi maalum cha watoto wa
kike kupatiwa mafunzo ya namna ya kujilinda.
Matukio mengi ya wanafunzi kupata ujauzito yamekuwa yakihusishwa
na mazingira yasiyo rafiki ya shule wanazosoma ukiwemo umbali wa shule
na wengine kulazimika kuishi kwenye nyumba za kupanga kilio ambacho kila
mara kimeelekezwa kwa serikali kuharakisha mpango wa ujenzi wa hosteli
hususani katika shule za kata .
0 comments:
Post a Comment