Wednesday, October 1, 2014

NGO’S YAENDESHA MAHAKAMA YA WAZI

23
Jenerali Ulimwengu ambaye ndiye mwezeshaji  akiendelea kutoa Mwongozo katika mkutano wa siku mbili juu ya mabadiliko ya Tabianchi, uhakika wa Chakula na haki za Ardhi mkutano ulioandaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC.
********
Na Mwandishi wetu
MTANDAO wa Asasi zisizo za Kiserikali zinazojishughulisha na masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi (ForumCC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Oxfam, zimeendesha mahakama ya wazi kwa lengo la  kufikisha ujumbe na kuonyesha tatizo hilo lilivyo nchini.
Mahakama hiyo iliendeshwa jana kwa muda wa saa tisa katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kuongezwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Richard Mziray na wasaidizi wake Jonas Lyakundi na Emmael Lukumai.
Mbali na tabia ya nchi pia mada nyingine kuu nyingine zilizoongoza usikilizwaji wa kesi hizo ni Haki ya Chakula na upatikanaji wa ardhi ambapo wawakilishi kutoka mikoa mitano iliyokithiri kwa kesi za migogoro ya ardhi walitoa kero zao.
Jaji Mziray alisema, hatua hiyo iliyofanywa na mashirika hayo yanapaswa kuigwa kwa kuwa sio watu wote wenye uwezo wa kivifikia vyombo vya haki.
Naye Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa, alisema wameamua kufanya hivyo ili kuileta jamii iliyokata tamaa pamoja.
1
Robert Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu mabadiliko ya Tabianchi.
Alisema kuwa wamealika wadau mbalimbali ili kufikisha ujumbe kwa haraka ambapo walialika Serikali, vyombo vya sheria, Taasisi na Asasi za kiraia ili kuonyesha ni namna gani masuala haya yalivyokuwa ni tatizo na yamekuwa yakiathiri moja kwa moja mfumo wa maisha na kurudisha nyuma maendeleo .
Alisema ni lazima kutafuta namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, jinsi ya kufanya mfumo wa  chakula uwe wa haki na usawa kwa wote na umuhimu wa ardhi pamoja na namna ya kutatua changamoto zake hususani katika uwekezaji na umiliki ardhi.
Naye Meneja Kampeni wa Oxfam alisema mahakama hiyo ni njia mbadala ya kuwaleta wanajamii wanaokereketwa kwenye jukwaa la pamoja ambalo watapata fursa na kubadilishana taarifa, ushauri na ufafanuzi.
Ester Kulwa mama Shujaa wa Chakula kutoka Mwanza, alisema Serikali imekuwa ikitumia uelewa mdogo wa wananchi walionao katika masuala ya kumiliki ardhi na kuamua kuwapoka wananchi ardhi yao jambo ambalo limekuwa likiibua mifarakano kila kukicha.
10
Meza  ya Majaji wakiwa wanasikiliza kwa makini malalamiko ya walalamikaji kutoka Loliondo juu ya kuchukuliwa ardhi pamoja na Malalamiko kutoka Wilaya ya Kishapu.
8
Kushoto ni mmoja wa walalamikaji kutoka Loliondo akielezea kwa uchungu jinsi Muwekezaji alivyo wanyang’anya Ardhi yao na mpaka sasa hakuna kitu ambacho kinaendelea na wanahitaji kupata Msaada wa kisheria ili wapate rudishiwa Ardhi yao.
16
Kushoto ni Mama kutoka Loliondo akitoa malalamiko yake Mbele ya Mahakama ya wazi Jinsi mwekezaji alivyochukua Ardhi, kusababisha uharibifu na akina mama kuteseka pamoja na wengine kuharibu Mimba zao pia kupoteza watoto ambapo mpaka sasa kuna mtoto hajaonekana.
19
Mlalamikaji Mwengine kutoka Loliondo akielezea Mbele ya Mahakama ya wazi  jinsi ya eneo lao lilivyochukulia na mwekezaji, na kutaka agizo la Mh. Waziri Mkuu lifanyiwe kazi la kwamba ardhi ile ni ya wafugaji na wanatakiwa warudishiwe.
21
Mmoja wa walalamikaji kutoka Wilaya ya Kishapu akitoa malalamiko yake mbele ya Mahakama ya wazi juu ya walivyo chukuliwa maeneo kwa ahadi ya kuyaendeleza na kuto fanya hivyo, na kuomba eneo hilo ambalo ni mashamba warudishiwe ili waendelee na kilimo kwa kuwa eneo hilo kuna shida ya njaa.
27
Mchangiaji kutoka Oxfam Bwana Marc akizungumza juu ya haki za binadamu na moja ya haki hizo ni haki ya kila mwanadamu kuwa na Chakula, na kuongezea kuwa hata Umoja wa Mataifa unafahamu hilo Pia amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mtu kujua sheria za umiliki wa Ardhi.Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada.
28
Mjumbe wa Bodi kutoka Forum CC akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mmoja wa wachangiaji akizungumza Jambo.
Mh. Jaji Richard Mzilay akitoa maelezo ya kina juu ya walalamikaji kutoka Loliondo ambao walikuwa wana malalamiko ya Ardhi na Kishapu ambapo walikuwa wanataka eneo lao lirudishwe, ametoa maelekezo ya yale ambayo wanatakiwa wayafuate.
18
20
5
Washiriki wa mkutano huo.
Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada
Burudani elimisha ikiendelea
Wadau wameguswa na kujumuika kucheza.
33
Picha ya pamoja.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI