HATIMAYE mahakama ya wilaya ya bunda mkoani Mara imewachia kwa
dhamana viongozi na wanachama kumi wa chama cha Demokrasia na
maendeleo Chadema baada ya kusota mahabusu kwa siku sita kufuatia kesi
ilifunguliwa na jeshi la Polisi kwa kudaiwa kufanya mkusanyiko
kinyuime cha sheria na kuhatarisha amani.
Wakizungumza muda mfupi baada ya viongozi hao sita wakiwemo
wanachama wanne wa Chadema na CCM kupata dhamana hiyo kwa kusimamiwa
na mawakili kutoka kampuni ya mawakili ya Ap ya jijini Mwanza, viongozi
baadhi ya Chadema mkoa wa Mara na wilaya ya Bunda, wamedai kusikitishwa
na nguvu kubwa zinatumiwa na vyombo vya dola dhidi ya vyama vya
upinzani.
Hata hivyo mmoja ya mawakili hao kutoka katika kampuni ya uakili ya
Ap ya jijini Mwanza Bw Afred Goyayi ameishukuru mahakama hiyo ya wilaya
ya Bunda kutenda haki kwa kukubali maombi ya dhamani kwa watuhumiwa
hao baada ya upande ya mashitaka kuweka pingamizi kuhusu dhamana hiyo.
Septemba 23 mwaka huu jeshi la Polisi liliwakamata viongozi na
wanachama hao wa Chadema na CCM kwa madai ya kufanya maandamano ambayo
yalizuiwa na jeshi la Polisi kisha kufunguliwa mashitaka ya kufanya
mkusanyiko bila kibali kinyume cha sheria na kuhatarisha amani, kesi
hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo oktoba saba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment