| ||
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria
Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula Bw. Charles wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam.
Picha na Georgina Misama
*****************************
|
Frank Mvungi, MAELEZO, DAR
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa
wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo kwa
wakulima baada ya kuiuzia nafaka Serikali.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari,
jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa
na wakala huo.
Walwa alisema kuwa wakala huo umeweza kuongeza kiasi cha nafaka
zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka tani 61,587.784 mwaka
2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa
kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.
“Hadi kufikia Desemba 31 mwaka 2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za
nafaka sawa na asilimia 110 ambapo tani 218,878.600 ni mahindi na tani 498.682
ni mtama” alisema Walwa.
Aliongeza kuwa wakala umeingia makubaliano ya mashirikiano (Memorandum of Understanding (MOU) na Shirika la Mpango wa
Chakula Duniani (WFP) ili kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.
Katika kutekeleza makubaliano na WFP Walwa alisema
kuwa wakala umeuza tani 80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa wakala
unaendelea kutekeleza mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka
2013/2014.
Katika hatua nyingineWalwa alisema kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya
nafaka kutoka kwa wananchi, ajira za muda kwa wananchi takribani
3000 zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakati wa kukusanya nafaka
tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula umepanga kuongeza uwezo wa
kuhifadhi nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa hadi tani laki 400,000
ifikapo mwaka 2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.
0 comments:
Post a Comment