Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi.
Action
Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na
mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa
ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa
weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani
Mafunzo
yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita,
kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za
asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya
mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo
hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa
Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za
Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo
haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu
za kujiunga na mafunzo.
0 comments:
Post a Comment