Saturday, March 1, 2014

CHANZO CHA KIFO CHA MUIGIZAJI NCHINI MAREKANI PHILLIP SEYMOUR CHAJULIKANA

Matokeo ya uchunguzi uliofanyika juu ya kifo cha aliyekuwa mshindi wa tuzo maarufu nchini marekani za oscar, muigizaji Philip Seymour Hoffman yameeleza kuwa muigizaji huyo alifariki kutokana na kuzidisha ubwiaji wa madawa ya kulevya kadhaa kama.
Ofisi ya mtabibu jijini New York ijumaa ya wiki iliyopita iliweka wazi kuwa mchanganyiko huo wa sumu ulitokana na kuchanganya madawa ya kulevya ambayo ni heroin, cocaine, benzodiazepini na amphetamine
Ambapo kwa kawaida Benzodiazepini hutumiwa kutibu hali ya kuwa na wasiwasi au usingizi, wakati pia amphetamine ni dawa kali na inayomfanya mtu kutamani itumia kwa muda wote. 

Hoffman alikutwa amekufa akiwa na sindano mkononi mwake, nyumbani kwake West Village katika jiji la New York mnamo tarehe mbili mwezi wa pili

Ukaguzi ulifanyika katika nyumba yake na kugundulika alikuwa na mifuko 70 ya heroin, chupa kadhaa ya dawa za tiba, na zaidi ya sindano ishirini zilizotumika zikiwa zimewekwa katika kikombe cha plastiki.
Wiki mbili zilizopita, waraka wa urithi ulioachwa na marehemu Hoffman ulisomwa ambapo yeye mwenyewe hakupenda mwanae aitwaye Cooper akue jijini Hollywood

Donald Sutherland (kushoto) akiwa na marehemu Phillip Seymour (aliyesimama) katika filamu hiyo ambayo msimu huu iliitwa Catching Fire

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI