Ofisi ya mtabibu jijini New York ijumaa ya wiki iliyopita iliweka wazi kuwa mchanganyiko huo wa sumu ulitokana na kuchanganya madawa ya kulevya ambayo ni heroin, cocaine, benzodiazepini na amphetamine
Ambapo kwa kawaida Benzodiazepini hutumiwa kutibu hali ya kuwa na wasiwasi au usingizi, wakati pia amphetamine ni dawa kali na inayomfanya mtu kutamani itumia kwa muda wote.
Hoffman alikutwa amekufa akiwa na sindano mkononi mwake, nyumbani kwake West Village katika jiji la New York mnamo tarehe mbili mwezi wa pili
Wiki mbili zilizopita, waraka wa urithi ulioachwa na marehemu Hoffman ulisomwa ambapo yeye mwenyewe hakupenda mwanae aitwaye Cooper akue jijini Hollywood
Donald Sutherland (kushoto) akiwa na marehemu Phillip Seymour (aliyesimama) katika filamu hiyo ambayo msimu huu iliitwa Catching Fire |
No comments:
Post a Comment