Somo la kingereza nchini limekuwa gumzo kutokana na wanafunzi wa kada zote nchini kushindwa kufanya vizuri katika somo hilo jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya wanafunzi kulichukia somo hilo.
Kwa mfumo wa utoaji elimu nchini darasa la kwanza mpaka la saba wanafunzi wamekuwa wakijifunza masomo yote kwa lugha ya Kiswahili ukitoa somo lenyewe husika la kiingereza. Na mara tu mwanafunzi huyo anapojiunga na kidato cha kwanza mpaka cha nne basi hujikuta katika wakati mgumu kutokana na ukweli kwamba kila somo katika ngazi hii hufundishwa kwa lugha ya kiingereza, huku matokeo ya mitihani mbalimbali nchini yakiwa hayaridhishi.
Kwa kulifahamu hilo wanazuoni kutoka chuo kikuu cha dar es salaam pamoja na wadau wengine wa elimu nchini wanakutana katika warsha ya pamoja kujadili namna ya ufundishaji wa somo la kiingereza ambalo limekuwa likiwapiga chenga wanafunzi walio wengi nchini.
Katika kikao hicho Prof. Eustela Bhalalusesa ni Kamishna wa Elimu akazungumzia malengo ya warsha hiyo na sababu za somo la kiingereza kushindwa kufanya vizuri.
Wanafunzi walio wengi wamekuwa wakitoa lawama kwa madai kuwa mabadiliko ya mitaala imekuwa ikichangia kufanya vibaya kwa somo la Kiingereza.
Demetria Hyera ni Mkuza Mitaala kutoka taasisi ya Elimu Tanzania.
Kwa upande wake Daktari Aneth Komba ambaye ni Msaidizi wa kutoka Shule kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam alizungumzia umuhimu kufundisha somo la kiingereza na kusema kuwa kwa sasa dunia imekuwa kama kijiji kimoja, hivyo ni vizuri somo hili likatiliwa mkazo kwani litakuwa na manufaa hasa katika kuwasiliana na watu mbalimbali duniani.
0 comments:
Post a Comment