Thursday, November 22, 2012

RAIS KIKWETE AGUSWA NA WAGONJWA WA FISTULA

Rais Jakaya Kikwete akiwa na wafanyakazi wa CCBRT na Vodacom.
Idadi ya wagonjwa  wa fistula nchini inazidi kuongezeka kutokana na matatizo  ya uzazi wanayoyapata wanawake wakati wa kujifungua.
Hayo yameabainika baada ya rais jakaya mrisho  kikwete kutembelea ujenzi unaoendelea katika hospitali ya CCBRT, ujenzi uliofadhiliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom.
Taarifa zaidi na Abdallah salehe

Rais kikwete alipata fursa ya kutembelea wagonjwa katika hospitali hiyo ambayo imekuwa ikitoa msaada kwa wagonjwa wenye maradhi ambapo juhudi ya waganga na wauguzi inaonekana waziwazi kutokana na mchango wao wanaouto ikiwepo roho ya huruma kwa wagonjwa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya CCBRT  wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa hatari wa fistula pamoja na magonjwa mengine sugu.

Moja kati ya maradhi yanayoonekana kumfedhehesha mwanamke ni pamoja na ugonjwa wa fistula, ugonjwa ambao hakika unaoneka kumyima raha mwanamke na kufikia hatua ya kutengwa na jamii.

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mtoto mmoja katika hospitali hiyo ya CCBRT
Pamoja na juhudi zinazofanywa na hospitali hiyo lakini bado idadi ya wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa huo wa fistula wamefikia elfu thelasini na moja huku idadi kubwa ya wanawake wenye matatizo hasa ya uzazi wakati wa kujifungua.

Rais kikwete pia alipata fursa ya kutembelea majengo mapya  yanayojengwa kwa kushirikiana na kampuni ya vodacom, ujenzi ambao utaweza kusaidia kupokea idadi kubwa ya wagonjwa.

Bi. Janeti Mbene
Naibu Waziri wa Fedha Bi. Janeti Mbene alipata fursa ya kuelezea jinsi ujenzi wa majengo hayo mapya unavyoendelea na jinsi utakavyowanufaisha watanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Bw. Renemeza, akapata fursa pia ya kuelezea jinsi ujenzi huo umpya.
Shughuli hiyo ilihudhuliwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ambapo rais Kikwete alikabidhiwa hundi yenye thamani ya  Sh. bilioni Nane fedha halali za kitanzania,  fedha zilizochangishwa kwa ajili ya ujenzi huo utakaowasaidia wanawake wenye maradhi mbalimbali nchini.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI