Na Hilali Ruhundwa…
Katika kile kinachoonekana kuwa ni utekelezaji bora wa majukumu, pamoja na utendaji kazi kwa ufanisi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa serikali, Waziri wa uchukuzi Dkt. Mwakyembe, ameanza kuchukua hatua kwa vitendo dhidi ya watendaji wabovu, ili kuboresha huduma katika Bandari ya Dar es salaam.
Hatua hiyo ya waziri Mwakyembe kuwafuta kazi watendaji hao inakuja baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati aliyounda, kuchunguza utendaji kazi katika bandari ya Dar es salaam, Ripoti ambayo amekabidhiwa siku chache zilizopita ambapo aliahidi kuchukua hatua kwa vitendo, kutokana na uchunguzi uliofanywa na kamati hiyo, ahadi ambayo ameitimiza kwa kuwafuta kazi watendaji hao.
Waliofukuzwa kazi ni pamoja na Bw. Danstan G. Mrutu, Eng. George H. Ally, Bi. Maria N. Kejo, Mhe. Alh. Mtutura A. Mtutura (Mb), Bi. Mwantumu J. Malale na Bw. Emmanuel Mallya ambapo walioteuliwa ni Dkt. Jabiri Kuwe Bakari, Bw. Said Salum Sauko, Bw. John Ulanga, Bi. Caroline Temu, Bi. Asha Nassoro, Dkt. Hildebrand Shayo, Bw. Jaffer Machano na Mhandisi Julius Mamiro.
Kufuatia mabadiliko hayo Dkt. Mwakyembe ameiagiza uongozi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania(TPA) kukabidhi nyaraka kwa watendaji wapya walioteuliwa kabla ya siku kumi atakapokutana nao, kwa ajili ya kuingia mkataba wa ufanisi.
Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania(TPA) ni miongoni mwa maeneo ambayo yanatajwa kwa utendaji mbovu wa kazi, ambapo imekuwa ikiinyima serikali ya Tanzania mapato ya kutosha, kutokana na nchi zinazotumia bandari ya Dar es salaam kuihama na kutumia bandari zingine ikiwemo ya Mombasa nchini Kenya.
0 comments:
Post a Comment