Tuesday, November 8, 2016

RONALDO - ''NINA MIAKA KUMI BADO YA KUCHEZA SOKA REAL MADRID''

 MCHEZAJI Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid utakaomalizika Mwaka 2021, amesema anaweza kuendelea kucheza soka kwa miaka kumi zaidi baada ya kusaini mkataba huo mpya.
Ronaldo ambaye ana umri wa miaka 31 mkabata wake ulikua unamalizika mwezi Juni 2018, lakini mkataba mpya aliosaini utamuweka kwa miamba hao wa soka wa Hispania mpaka Juni 2021.
Mchezaji huyu amesema “Nilichokua nakitaka ni kuendelea kufurahia kucheza kwa miaka iliyobaki. na bado nina miaka kumi,”
Nyota huyu amefunga mabao 371, toka alipojiunga na Real Madrid akitokea Manchester United, mwaka 2009.

Ronaldo ameisaidia timu yake ya Real Madrid, kutwaa ubingwa wa ulaya mara mbili, ubingwa wa la Liga na mataji mengine.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI