Tuesday, November 15, 2016

MTANZANIA ASHIKA NAFASI YA NNE KATIKA SHINDANO LA UPISHI DUNIANI *PICHAZ*

President and CEO of WORLD FOOD CHAMPIONSHIP Mr Mike Mc Cloud akimkabidhi tuzo Uisso
MTANZANIA Fredy Uisso aliyekwenda Alabama, Marekani,kushiriki mashindano ya upishi ameibuka mshindi wa nne katika mashindano hayo ya kidunia.
Usiku wa kuamkia leo, Mkurugenzi Mtendaji wa World Food Championships Mike Mc Cloud, alimtangaza Uisso kuwa mshindi wa nne katika shindao hilo.
Chef Uisso ambaye ni mpishi mwandamizi katika mgahawa wa Afrikand uliopo Kinondoni, anaandika historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kushiriki fainali za mashindano hayo na kuibuka kuwa mshindi wa nafasi hiyo huku akiwabwaga wapishi 21 kutoka hoteli kubwa na maarufu duniani walioshiriki fainali hizo zilizoanza Novemba 8 mwaka huu.
Uisso akiwa na Madam Julie Haunn the National Coordinator WORLD FOOD CHAMPIONSHIP

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI