MSHAMBULIAJI wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya England, Harry Kane ameondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa baada ya kushindwa kufaulu vipimo vya utimamu wa mwili.
Kane mwenye umri wa miaka 23, aliitwa kwenye kikosi cha timu hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya kurejea uwanjani kuitumikia klabu yake ya Spurs ambayo ilimkosa kwa muda mrefu kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu.
Kocha wa England, Gareth Southgate amethibitisha kumuondoa Kane, na anaamini atakua fit katika siku zijazo ambapo ataita tena kikosi chake kwa ajili ya kuendelea na kampeni za kuwania kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment