Tuesday, November 15, 2016

OMMY DIMPOZ - 'KUNA BAADHI YA WASANII WANANUNUA VIEWS YOUTUBE'

MSANII wa muziki Ommy Dimpoz amedai kuna baadhi ya wasanii wananunua views katika mtandao wa YouTube ili video zao zionekane zimeangaliwa zaidi.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’ akiwa na Alikiba amedai yeye hawezi kufanya mchezo wa kununua views kama baadhi ya watu wanavyofanya.
“Mimi nataka kutoa wito maana siku hizi watu ‘wanachiti’ sana hususan kwenye mambo ya views YouTube,” Ommy alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM. “Mimi ningewaambia kitu kimoja fanya ngoma kali video acha watu waangalie,”
“kwa sababu naongea kwa uzoefu wangu mimi na video yangu ‘Wanjera’ ilikuwa na views laki tisa, kuna mtu mmoja akaniambia siwezi kumsema ni nani ila aliniambia bwana vipi unataka views YouTube? Nikamuuliza views YouTube kivipi, akaniambia hebu nitumie link ya video yako. So mimi nilikuwa nataka kuprove nikamtumia link ya ‘Wanjera’ na ilikuwa na views laki tisa na elfu nne hivi lakini baada ya kumtumia masaa sita baadae akaniambia angalia kuangalia nakuta na milioni moja,” alifafanua zaidi.
Muimbaji huyo amedai hatua hiyo ilimfanya agundue ni kweli kuna baada ya watu wananunua views YouTube.
Video mpya na muimbaji huyo aliyoshirikiana na Alikiba ina views 607,967 ikiwa na ina wiki moja toka iwekwe katika mtandao wa YouTube.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI