Tuesday, November 8, 2016

MESSI AFIKISHA BAO LA 500 BARCELONA

Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesheherekea tukio jingine la kihistoria baada ya kuifungia klabu yake bao lake la 500 siku ya Jumapili.
Messi ambaye saivi ana umri wa miaka 29 aliifungia Barcelona bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla.
Messi ameifungia Barca mabao 500 katika mechi 592,ikiwemo mechi za kirafiki huku mechi 469 zikiwa rasmi.
Messi sasa anakuwa amemshinda aliyekuwa na mabao mengi Paulino Alcantara ambaye aliichezea Barcelona katika vipindi viwili vya kati ya 1912 na 1927.
Mnamo mwezi Aprili,mshambuliaji huyo alifunga bao la 500,ikiwemo mechi za kimataifa,wakati Barcelona iliposhindwa 2-1 na Valencia.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI