Tuesday, November 15, 2016

CHEMICAL AFUNGUKA KUHUSU WIMBO WAKE ‘MARY MARY’ NA KUANDIKIWA NYIMBO ZAKE

RAPPER Chemical amefunguka kuhusu idea ya wimbo wake mpya wa ‘Mary Mary’, kuachia nyimbo tatu kwa kipindi kifupi, pamoja na kuandikiwa nyimbo zake.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, rapper huyo amesema:
Kuhusu idea ya ‘Mary Mary’
Kitu kilichonifanya kuandika ‘Mary Mary’ ni kwa sababu yale maisha yapo, inawezekana sisi tunaishi huku tunafurahi tunajua pakula, tunajua pakulala lakini kuna watu wapo huko hawajui kula yao wala watalala wapi na wameshazoea yale maisha, wakila sawa na wakiamka sawa. Ni vitu tunavyoonana navyo kila siku, watoto wa mtaani wapo na tunawaona sehemu nyingi lakini inawezekana tuna ignore kwa sababu na sisi tumeshaona ni hali ya kawaida kitu ambacho si kweli. Kwa hiyo hii ngoma nimeandika ili kuwapa moyo watu wanaopitia maisha yale yatakuwa sawa na kuwafanya waamini kuna watu walipitia maisha yale lakini sasa hivi wanamaisha mazuri.
Kuhusu kuachia nyimbo tatu mfululizo
“Mary Mary” ndio project rasmi imefuata baada ya “Am Sorry Mama”, “Kama Ipo Ipo Tu” nimeitoa kwa sababu tulipanga mfumo, sisi kama Kazi Kwanza tutatoa videos za audio ambazo tushazitoa lakini hazikupata nafasi ya kufanyiwa video. Ni ngoma tatu zina mahadhi tofauti, ukiangalia “Am Sorry Mama”, “Mary Mary” na ukiangalia na “Kama Ipo Ipo Tu” ni ngoma tatu kwangu mimi naona zipo tofauti sioni kama kuna kitu kinaweza kuifanya hii kuishusha nyingine. Lakini kitu kingine mimi nahisi kama bado sijakuwa msanii yule wa kusema kwamba nikitoa nyimbo baada ya miezi sita ndio nitoe nyingine nahisi kama nakuwa kwa hiyo watu bado waendelee kumsikiliza Chemical mpaka ambao labda bado hawajaamini waamini ‘Yaah! I can do it’, ndio maana muda mwingine nakuwa najitahidi nisikae muda mrefu sana sijaachia nyimbo.
Kuhusu kuandikiwa nyimbo
Ngoma zote naandikaga mwenyewe, sio kama sipendi kuandikiwa na mtu au vipi, no ni kwa sababu hicho kipaji ninacho cha kuandika, sidhani kama ukiwa na kipaji cha kuandika lazima uende ukaandikiwe na mtu mwingine wakati you can do it. Kwahiyo mimi naweza kuandika ndio maana naandika mwenyewe. Lakini ikitokea mtu akaniandikia wimbo akaniletea na nikaona kweli ni nzuri na ninaweza kuutumia, nitautumia kwa makubaliano maalum. Lakini kitu kingine kinaniogopesha kuandikiwa nyimbo mara nyingi unakuta mimi nina style yangu na flow zangu kwa hiyo nikiwa naandika wimbo huwa naandika as Chemical lakini mara nyingi ukiandikiwa na mtu either anaandika kwa hisia zake au anaandika kwa flow zake, sana sana kwenye Hip Hop. Mimi nikiandika naandika kwa flow zangu kwa hiyo inawezekana ukiniletea ngoma lazima nitaibadilisha iwe kwenye flow zangu haiwezi kuwa kwenye flow zako lakini all in all akitokea mtu mzuri wa kuniandikia akanionyesha kwamba Chemical hii nyimbo inakufaa nikaona kweli inanifaa basi niko tayari kufanya hivyo.
#Bongo5

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI