Sunday, October 25, 2015

MHE. EDWARD LOWASSA (CHADEMA) APIGA KURA MONDULI…ASEMA ANATEGEMEA USHINDI NA HATAKUBALI MATOKEO IWAPO YATAHUJUMIWA *PICHAZ*

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Edward Lowassa amepiga kura, Monduli.
Lowassa alipata nafasi ya kujibu maswali kadhaa ya waandishi ambao walitaka kujua nini matarajio yake baada ya matokeo ambapo jibu lake lilikuwa ni 'Ushindi'.
Lakini pia kama atakuwa tayari kutakubali matokeo iwapo atashindwa ambapo Lowassa amesema atakubali matokeo kama hayatachakachuliwa, vinginevyo hatakubali.
Waandishi pia walitaka maoni ya Lowassa kuhusu hukumu ya mahakama kukataza watu kukaa mita 200 baada ya kupiga kura.
Katika majibu yake, Lowassa amesema hali aliyoiona kituoni ni ya amani na utulivu hivyo hana maoni ya ziada kuhusu hukumu ya kukaa mita 200

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI