Tuesday, September 8, 2015

ANGALIA *VIDEO* YA KUBENEA AKIFUNGUKIA DR. SLAA KUHUSU RICHMOND NA MENGINE MENGI


Hapa  kuna  video  ya  Kubenea  akimchanachana  Dr.  Slaa  katika  mkutano  wa  hadhara  Kyela, Mbeya.

  1. Amesimulia  sakata  zima  la  Richmond  kwa  kudai  kuwa  wakati  likiwakilishwa  bungeni  kulikuwa  na  ripoti  mbili. Moja  ya  kumchafua Lowassa  na  ya  pili  ikidai  Kikwete  ndo  mhusika  wa  Richmond
  2. Amesema  aliyekuwa  akipinga  ujio  wa  Lowassa  Chadema  ni  Baregu  na  siyo  Dr Slaa.
  3.  Amesema  kamati  kuu  ya  chadema  ilijiridhisha  kuwa  Dr  Slaa  asingeweza  kushinda  uchaguzi  wa  mwaka  huu  kama  angesimamishwa  kuwa  mgombea  wa  urais
  4. Amedai  kilichomponza Slaa  ni  mkewe  ambaye  alikuwa na uchu wa kuwa first lady 
  5. Baada ya hapo,Slaa  alianza  kampeni  za  kumpinga Lowassa  ili  ateuliwe  yeye. Alimtuma Sugu  aende Mbeya  akawaambie  waumini wa makanisa yote kuwa wao wanamtaka  Slaa  na  sio  Lowassa, lkn  Sugu  Alikataa. 
  6. Slaa  pia  alijaribu  kumrubuni Tundu Lissu  atangaze kumpinga Lowassa  lakini  naye  alikataa  pia  na  kujikuta  akibaki  peke  yake, hali  iliyomfanya  ajivue  uanachana 
  7. Amesema  Slaa  alikuwa Padri  akaasi,alikuwa na mke akaasi, alikuwa CCM akajitoa, je ana principle gani za kuwashawishi watanzania  wamuamini? 
  8.  Dr Slaa  ni msaliti na anatumia umaarufu wake vibaya 
  9. Slaa anadai kuwa nyaraka za Richmond alipewa na Mwakyembe, lakini ukweli ni kuwa mwakenye hawezi  kuwa mtu sahihi  wa  kutoa  nyaraka  za  Richmond  kwa  sababu  wakati  wa Ripoti  hiyo, Mwakyembe  alikuwa na kampuni yake  ya  kufua  umeme  ambayo  alitaka  ipite. Baada  ya  kukwama  ndo  akaanza ugomvi na Lowassa 
  10. Tazama video hapo chini kumsikiliza  akifunguka

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI