Tuesday, December 23, 2014

UGOMVI WA KOFIA ULIENDA MBALI ZAIDI, MKASI UKATUMIKA KUYAKATISHA MAISHA YA MTU …

29877241.Monday7thJune2004
UGOMVI wao ulianza kama utani, mmoja hakupendezwa na utani huo, hata alipokasirika mwenzake alidhani utani unaendelea, Agwugho akajikuta akifanya maamuzi ambao yalipelekea rafiki yake kufariki.
Polisi wa Lagos, Nigeria wamesema wamemkamata mtuhumiwa Joseph Agwugho kwa tuhuma za kumuua rafiki yake Enya Okpara, kwa kumchoma na mkasi rafiki yake, uchunguzi unaonyesha Agwugho na Okpara walikuwa wakigombania kofia ndipo mtuhumiwa alipochukua mkasi na kumchoma nao marehemu shingoni mara tatu.
Okpara alikimbizwa katika Hospitali  Lagos na muda mfupi baadaye kufariki, Agwugho anakabiliwa na kesi ya mauaji, alipandishwa Kizimbani na baadaye kurudishwa gerezani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI