Tuesday, November 15, 2016

MADEE - 'DOGO JANJA BADO HAWEZI KUJISIMAMIA'

MMOJA kati ya viongozi wa juu wa Tip Top Connection, Madee amedai rapa Dogo Janja bado hajakuwa kwa kuweza kujisimamia katika muziki wake.
Madee amesema rapa huyo hawezi kuondoka Tip Top Connection bila ruhusa ya uongozi wake kwa kuwa tayari alisharubuniwa na akaona madhara yake.
“Wao ambao wanataka kufanya biashara na Dogo Janja kabla ya kuongea na Dogo Janja basi waufuate uongozi wa Tip Top hasahasa Madee lakini sio yeye juu kwa juu kwa sababu mimi siamini kama Dogo Janja anaijua biashara yake kwa sasa hivi,” Madee aliambia 255 ya Clouds FM.
Aliongeza, “Mimi bado namuona Dogo Janja bado ni mtoto, hawezi kurubuniwa ndio maana mwanzo alivyorubuniwa na wale ambao walimrubuni walifanikiwa lakini mwisho wa siku Dogo Janja aliona madhara yake. So sidhani kama atakuwa na akili za kijinga jinga kama mwanzo za kukurupuka,”
Dogo Janja kwa sasa anafanya vizuri na wimbo Kidebe.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI