STAA wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Lulu alisema akiwa na mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.
“Masharobaro hawana nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha kabisa, hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro,” alisema Lulu.
0 comments:
Post a Comment